Watuareg ni kabila ambalo limeishi katika jangwa la Sahara kutoka miaka mingi. Targui ni mwanachama wa kabila hili na Tuareg ni neno linalotumika kwa ajili ya kutaja kundi nzima, lakini wao wanajiita kel tamasheq yanayomaanisha “wanaosema Kitamasheq.” Kitamasheq ni lugha yao. Inadhaniwa kwamba neno la Tuareg lilitumika kwa mara ya kwanza na Ibn Khaldun. Hilo linamaanisha “watu ambao wametelekezwa na Mungu” (Raffray, 2013: 5.). Nafikiri kuwa maana hii ni matokeo ya aina ya Uislamu uliofika eneo hili na pia kwa sababu Watuareg waliubadili Uislamu huo na kuuchanganya na desturi zao.
Jamali, mavazi na hema ni muhimu sana kwa jamii hilo. Ngamia ni mnyama anayependekezwa mno. Mtu anayekuwa na jamali wengi anapewa heshima za kijamii kwa sababu ndiye anayeruhusiwa kutetea umma. Matendo hayo yanafanyika wakati kundi jingine likiwashambulia Watuareg. Pia jamali ni muhimu kwa ajili ya biashara, kwa hivyo Watuareg wanapohitaji chochote wangesafiri katika misafara ya jamali kwa sababu ngamia ni mnyama avumiliaye hali ya hewa ambayo huwa joto na kavu. Kuendelea, kuhusu mavazi, vyandalua wanavyovaa vina heshima sana. Kwa kawaida, baba anamvalisha mtoto wake wa kiume chandalua na hivyo ni ibada ifanyayo huko mtoto akiwa anapita kutoka utotoni hadi uzima. Kutokana na mawazo ya Watuareg, kuonyesha uso ni kitendo kinachowabumbuaza watu, zaidi ya yote kwa sababu vyandalua ni vitu vinavyowaunganisha Watuareg na wahenga wao. Hema lina thamani sawa na chandalua, lakini hema ni kwa wanawake sio wanaume. Hema ni ishara ya nguvu waliyonayo kwao na kwa kawaida mama anampa binti yake hema (Bourgeot, 1990).
Kila mwanachama wa umma ana kazi tofauti, lakini kazi zote zina thamani. Amenokal ni watu ambao huongoza kundi la Watuareg na kuwadhibiti watu wa kundi lao. Imushaq ni wapiganaji wa vita na kwa kawaida pia wana jamali na kondoo wengi, hawa wa mwisho walikuwa muhimu ili kuwalisha watu na kwa ajili ya kuwadhibiti. Illelan ni watu wenye uhuru na Imghad ni wanaowalipa wakuu kodi. Inhaden ni wafundi au wahunzi ambao walisaidia kutatua matatizo baina ya makabila walipopambana na pia kuhifadhi mila ya mdomo. Ineslemen au marabout wana mamlaka ya kidini, majaji, washauri wa kisiasa na walimu wa madrasa au shule za Koran. Iklan ni watu wanaotoka kwenye familia za watumwa, lakini ni wanachama wa familia na Watuareg na watu wengine wanawasharifu (Lecocq, 2010. Duveyrier, 1864, Bernus, 2002).
Kabla ya ukoloni, Watuareg walihamia na kusafiri kote jangwani bila matatizo na kwa uhuru, kwa sababu kulikuwa hakuna mipaka jangwani, lakini Wazungu waliumba mipaka na kitendo hiki kimeharibu maisha ya Watuareg kwa sababu kuhamahama kuliwaruhusu kupata chakula walichohitaji. Jinsi wanavyoishi ni tofauti ya sisi. Nadhani kwamba Watuareg wasingalikuwa na matatizo mengi maisha yao yasingalikuwa yamebadilishwa na ukoloni.
Watuareg wanafikiri kwamba jangwa ni rafiki yao. Kwa ukweli kuna hadithi ya Watuareg isemayo kwamba kabla ya Watuareg watu wengi walijaribu kuishi jangwani, lakini wakati huo jangwa liliwaambia “huko kuna joto na baridi sana na hakuna maji mengi” na watu waliamua kuendelea na kutokaa huko. Watuareg walipofika, jangwa liliwaambia maneno yale yale ambayo yalikuwa yamesemwa kwa makundi mengine ya binadamu, lakini Watuareg walijibu kuwa wao walikuwa na vyandalua na kwamba jangwani kulikuwa na visima ili wanywe maji. Jangwa liliwaambia pia kwamba kulikuwa na mahali pa utulivu, lakini hilo halikuwa tatizo kwao. Jangwa liliwauliza “mnatarajia nini?” Na wao walijibu kuwa waliyokuwa wanayatafuta ni amani, uhuru na nguvu dhidi ya maadui yao. Jangwa liliwaahidi wangeweza kuwa na wanayotaka watakapoishi pamoja naye. Ndivyo, mkataba ulifungwa baina yao (ag Assarid, 2006).
Sasa Watuareg wanaendelea kuishi jangwani. Nafikiri katika siku zijazo wataendelea kukaa huko. Sasa hawana uhuru wa kuhamiahamia kama jinsi wanavyotaka kwa sababu jangwani kumegawanyika baina ya serikali tano. Nchi ambapo Watuareg wanaishi ni Mali, Aljeria, Nijeri, Libya na Burkina Faso (Lecocq, 2004). Utambulisho na utamaduni zao zimebadilika kutokana na mazingira tofauti wanayoishi kama utambulisho na utamaduni wa kila mtu.
Marajeo
Lecocq, B. 2004. ‘Unemployed Intellectuals in the Sahara: The Teshumara Nationalist Movement and the Revolutions in Tuareg Society’ International Review of Social History 49, 12: 87-109.
Raffray, M. 2013. Touaregs. La révolte des hommes bleus 1857-2013. París, Economica.
Bourgeot, A. 1990. ‘Identité touarègue: De l'aristocratie à la révolution’, Études rurales 120: 129-162.
Lecocq, B. 2010. Dispute desert. Decolonisation, competing Nationalisms and Tuareg Rebellions in Northern Mali. Leiden, Brill.
Duveyrier, H. 1864. Les Touareg du nord, Paris, challamel ainé.
Bernus, E. 2002. Les Touareg, Paris, Vents de sable, 2002.
Ag Assarid, M. 2006. En el desierto no hay atascos. Un tuareg en la ciudad, Barcelona, SIRPUS.