Ujamaa ulikuwa wazo wa kisiasa wa rais Julius Nyerere, aliyekuwa rais wa kwanza wa Tanganyika, kwa hivyo siasa ya ujamaa ilianza baada ya Tanganyika kupata uhuru. Nyerere alitaka kuboresha uchumi wa Tanganyika. Ili afanye hivyo Nyerere alitaka kilimo kiwe kitendo kikuu cha uchumi wa nchi. Mambo hayo yalikuwa magumu ili yafanyike. Mpango wa vijiji vya ujamaa vya Tanganyika ulikuwa viwe kama kijiji cha hadithi hiyo kinachoitwa “Nipe Nikupe”.
Rais wa Tanganyika alitaka nchi yake ianze kuongeza mazao yake ya kilimo. Kwa hivyo mnamo mwaka elfu moja mia tisa sitini na saba aliandika Azimio la Arusha1 ili apange Tanzania jinsi itakavyokuwa katika wakati ujao. Azimio la Arusha lilieleza siasa ya ujamaa, huko likisema kwamba mali ya mashamba yatabadilika yawe mali ya wakulima wote wa kila kijiji.
Serikali ya Tanzania ilijikuta na mapinzano makubwa kwa sababu katika utamaduni wa Watanzania kwa ujumla kulikuwa na sehemu mbili tu, Rungwe na Sumbawanga, ambapo waliishi katika vijiji vilivyofanana na vijiji vya ujamaa2. Kwa hivyo, kujenga vijiji kulikuwa muhimu mno katika wakati wa ujamaa kwa sababu mahala ya mashamba yalikuwa mbali na hapakuwa rahisi kuendeleza kilimo katika sehemu hizi zote3. Ujamaa ulikuwa umefuatia wazo ya Rungwe na Sumbawanga lakini wakulima hawakubadili kwa haraka na wengine hawakutaka kubadili moja kwa moja.
Nyerere alitaka kujenga vijiji kwa sababu Tanzania ilihitaji pesa zitokazo nchi zingine ili kupata teknolojia bora ya kilimo na kadhalika. Mpango wa ujamaa ulitegemea sana wakulima wa Tanzania kwa sababu serikali ilitaka iwaongoze wakulima lakini bila kuwaambia wafanyeje moja kwa moja4.
Wanahistoria wengi wanasema kwamba uchumi ni ujuzi uliotoka kwa watu waliojifunza nje ya Afrika. Uchumi wa wakati kabla ya Wazungu kufika Afrika ulikuwa kama ule wa kijiji cha “Nipe Nikupe.” Wazungu walipoanza ubepari na Waafrika walianza kujifikiria wao wenyewe tu. Nyerere alidhani kwamba kulikuwa lazima Watanzania wafanye kazi pamoja kama zamani5.
Nyerere alitaka Watanzania wenye adabu kwa hivyo Kiswahili kilianza kutumika shuleni, pia alifanya bidii ili wakulima wawe na shule za sekondari. Walimu wa mashule hayo walifundisha maarifa ya kilimo kwa sababu shule zilikuwa zinafuata maarifa ya Chama cha Mapinduzi6.
Ujamaa ulianza kuwa na matatizo mengi mnamo mwaka elfu moja mia tisa sabini na tano. Mwaka huu kulikuwa na njaa Tanzania kwa hivyo ilikuwa lazima kuingiza tani elfu ishirini na tano ya mahindi nchini kutoka nchi za nje7. Njaa ilisababisha watu wengi wawe kama Kunganyira baada ya kumpata kanga wake.
Serikali ya Tanzania ilijaribu kubadili uhusiano kati ya wakulima, kazi za kulima na mazao nchini Tanzania lakini haikuweza kufanya hivyo isipokuwa mara chache. Mara nyingi Ujamaa haukufikia hatua ya mwisho katika maendeleo yake lakini kuna vijiji vilivyokuwa na duka la kijiji au shamba kubwa ili watu wawe na kazi, ijapokuwa mali ya binafsi bado ilikuwa chango la kawaida sana. Ujamaa haukuwa na mafanikio hasa kwa sababu wakulima walitaka pesa na walikuwa kama Kunganyira.
Haji Gora Haji alimtumia mhusika wa Kunganyira ili aonyeshe hasara ya ukoloni, kwa sababu yeye aliacha kuwafikiria majirani wake na sasa alijifikiria mwenyewe tu. Ni lazima msomaji aone kwamba watu wote wanaoishi katika hali ya ujamaa ni lazima wakumbuke jina la kijiji cha hadithi hiyo “Nipe Nikupe.”