Mazungumzo (Conversación) 2

Mazungumzo ya Salif Keita


J.- Hamjambo? Mmeona kwamba Salif Keita atatembelea Mehiko?
G.- Sijambo! Ndiyo, nimeshaona kwamba Salif Keita atafanya maonyesho hapa mjini.
A.- Sijambo! Hapana, sikuyaona. Maonyesho yake yatakuwa wapi?
J.- Maonyesho hayo yatakuwa katika jumba la kucheza la mjini.
G.- Na maonyesho hayo yatakuwa tarehe gani?
J.- Yatakuwa tarehe kumi na saba mwezi wa tatu.
A.- Loo! Nimeshaona kwamba katika twitter kuna tiketi zinazotolewa bure.
J.- Mnataka kuenda kumwona akicheza?
A.- Ndiyo, nitapenda sana kuenda kumwona kwa sababu sijawa na nafasi ya kumwona akicheza kamwe.
G.- Ndiyo! mimi pia ningependa kuenda kumwona. Tutafanyaje ili tupate tiketi za bure?
A.- Inatubidi tuandike katika twitter “ninataka tiketi ya maonyesho ya Salif Keita” na kungojea jibu.

Baada ya kuandika katika twitter na kupata barua wanakutana kwa mara ngine.

J.- Gaby vipi? Nimeshaandika na nilipokea barua ya mtandao. Sasa nina tiketi mbili ni lazima niwape jina langu na kuonyesha kitambulisho changu nifikapo jumba la kucheza la mjini.
G.- Nzuri, mimi pia nimeshaandika na nimepewa barua ya mtandao. Je, Adriana na wewe umepokea barua hii?
A.- Hapana, ninafikiri kwamba nina bahati mbaya, sijapata barua lolote.
G.- Usiwe na wasiwasi, nitakuwa na tiketi mbili kwa hivyo nitaweza kupa tiketi nyingine.
J.- Tutafikaje huko?
A.- Tunaweza kuenda kwenye reli za chini ya ardhi yaani metro. Jumba la kucheza lipo karibu na kituo cha “Bellas Artes”.
G.- Lakini Javier ana gari mpya. Javier wewe unaweza kutubeba hadi jumba hilo na baada ya maonyesho utaturudisha nyumbani kwetu, siyo?
J.- Sina gari. Lazima ukumbuke kwamba haukutaka kuniuzia gari lako na kwa hivyo sina gari. Itatubidi tuende katika metro na baada ya kumsikiliza Salif Keita tutaenda kunywa pombe na kuzungumza kuhusu maonyesho.
A.- Sawasawa. Maonyesho yataanza saa ngapi?
G.- Maonyesho yataanza saa mbili kamili usiku. Tutaweza kuonana mbele ya jumba ili tuingie pamoja ndani.
A.- Tutaonana huko. Hapana Javier, sitaki kunywa pombe baada ya maonyesho kwa sababu tutakuwa na darasa siku ifuatayo, lakini tunaweza kunywa chokoleti.
J.- Ninapenda zaidi pombe, lakini tutaenda pamoja kunywa chokoleti na kuzungumza
G.- Tutaonana huko na tutaamua kufanya nini.
J.- Nitamwalikia rafiki yangu pia ili aende kumsikiliza Salif Keita. Kwa herini.
G y A.- Kwa heri.

Wafikapo kwenye jumba la kucheza.

J.- Hamjambo? Huyu ni rafiki yangu anayeitwa Roberto.
A.- Sijambo! Nimefurahi kukufahamu Roberto. Habari gani?
R.- Nzuri, asante. Nimefurahi kuwafahamu nyie pia.
G.- Sijambo! Tuingie kwenye jumba la kucheza ili tutafute viti vyetu!
R.- Tufanye haraka!
A.- Ndiyo, maonyesho yanakaribia kuanza.

Baada ya kuona maonyesho

A.- Je, mliyapenda maonyesho?
G.- Ndiyo, niliyapenda sana. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kumsikia Salif Keita akipiga muziki wake.
R.- Vivyo hivyo niliyapenda lakini siyo sana. Mimi ninapenda zaidi muziki wa reggae.
J.- Ndio, nimekubali Gaby. Kwangu mimi pia ilikuwa mara yangu ya kuanza kumsikiliza Salif Keita huko akifanya maonyesho. Mlipenda zaidi wimbo gani?
A.- Nilifurahia sawa nyimbo zote. Nilipenda sana mchanganyiko wa vyombo vyote vya muziki vilivyotumika.
G.- Niliweza kucheza dansi wakati wa maonyesho yote. Kulikuwa na watu wengi waliocheza pia.
R.- Nilikuwa sijawahi kuona watu wakicheza dansi ndani ya jumba hilo.
J.- Nilipenda sana wimbo unaoitwa “Madan” lakini sijui lugha ya wimbo huo. Nilitaka kucheza dansi lakini sikujua jinsi ya kuucheza.
A.- Mimi pia nilikuwa na wasiwasi kwa hivyo sikutaka kucheza, lakini miili ilikuwa inasogea kufuata mahadhi ya muziki jinsi ulivyokuwa unapigwa.
G.- Wanamuziki wa Keita walitumia ngoma mbalimbali, kwa mfano djembe na seti ya ngoma.
J.- Nilifikiri kwa kuwa zeruzeru yeye atakuwa na matatizo na mwanga, lakini nimesoma kwamba zeruzeru wana matatizo kutokana na jua tu.
R.- Nilikuwa sijawahi kuona wanamuziki wakiwaalika hadhara ulingoni ili wacheze. Ninafikiri kwamba Salif na wanamuziki wake ni watu wanyenyekevu.
A.- Sasa ninataka kujifunza kupiga kora. Nilipenda sana sauti yake, lakini sijui mahali ambapo ninaweza kununua kora au mwalimu atakayeweza kunifundisha.
G.- Inawezekana ninamfahamu mtu anayepiga kora, lakini sina uhakika. Nitamwuliza kesho. Niliwapenda waimbaji wawili waliofanya kiitikio cha Keita.
J.- Ufff! Mnaona? Ni saa tano kamili ya usiku na ni lazima tuende nyumbani.
A.- Ndiyo, kesho tutakuwa na darasa.
R.- Lakini metro imeshafungwa.
G.- Nilikuambia ulete gari lako Javier.
J.- Sina gari lakini Roberto atalipa teksi ili tuweze kurudia nyumbani.
R.- Ndiyo, ninaweza kulipa teksi. Pia ni lazima niamke mapema kesho kwa sababu nitafanya kazi.
A.- Haya tuende!

*Esta web está en continuo desarrollo, siendo actualizado su contenido periódicamente, por lo que progresivamente va ampliando el material publicado. 

colmex-swahililogo ceaa 50 

© 2015 El Colegio de México, A.C.