Mazungumzo (Conversación) 1

Mtihani - MazungumzoG- Hujambo Adriana?
A- Sijambo Gaby, habari za asubuhi?
G- Nzuri, habari za familia yako?
A- Nzuri, asante sana, ya kwako?
G- Nzuri sana, lakini nina tatizo.
A- Tatizo lipi?
G- Ni kwamba ninataka kuuza gari langu, lakini sijampata mnunuzi bado.
A- Labda ninaweza kukusaidia, unamkumbuka Javier?
G- Sina hakika, ni rafiki yako ambaye ni mrefu sana?
A- Ndiyo, sasa anatafuta gari kwa sababu shuleni kwake kupo mbali sana na nyumbani kwake.
G- Unaweza kumwuliza kama anataka gari langu?
A- Ndiyo, leo nitamwona shuleni na kumwuliza.

(Baada ya kufika shuleni)

A- Hujambo Javier?
J- Sijambo! Habari za leo?
A- Nzuri, asante. Unaendelea kutafuta gari?
J- Ndiyo, lakini nataka gari la bei nafuu kwa sababu sina pesa nyingi. Unamjua mtu anayetaka kuuza gari lake?
A- Ndiyo, asubuhi hii nilizungumza na rafiki ambaye nimefahamiana naye kutoka miaka mingi na huniambia kwamba anataka kuuza gari lake.
J- Baada ya madarasa ya leo, tungeweza kumtembelea rafiki yako?
A- Ndiyo, lakini ni lazima tule kabla ya kuenda.

(Wafikapo nyumbani kwa Gabriela)

A- Hodi Hodi.
G- Karibuni!
A- Starehe, habari za jioni?
G- Nzuri sana. Yeye ni rafiki yako anayetaka kununua gari?
A- Ndiyo Gaby, yeye ni Javier na anataka kununua gari, lakini hana pesa nyingi.
J- Hujambo? Ndiyo, mimi ni maskini. Unauza gari lililopo nje ya nyumba yako?
G- Sijambo. Ndiyo, gari hilo ndilo lile ninaloliuza, mnataka kuliangalia?
J- Ndiyo tafadhali.
J- Unaliuza bei gani?
G- Bei ya gari langu ni pesos elfu arobaini.
A- Mwaka ya gari lako ni upi?
G- Mwaka ya gari ni elfu mbili na tano.
J- Na lina kilometa ngapi?
G- Lina karibia kilometa elfu hamsini na tatu.
A- Umeshawahi kugongana na gari lingine?
G- Sijawahi kugongana na gari lolote wakati wote huo wa miaka kumi ambao nimekuwa na gari hili.
J- Lakini, hilo ni gari la kizamani. Kwa mfano magurudumu yake ni mabaya sana.
A- Ndiyo, ni lini mara ya mwisho ulipobadilisha magurudumu?
G- Nilibadili magurudumu miaka miwili iliyopita, lakini magurudumu ya nyuma ni bora zaidi.
J- Mtu ambaye ameyabadili hayo amekuibia au hujui kuendesha. Ni lazima niyabadilishe magurudumu kwa mara nyingine.
A- Ninafikiri kwamba Gaby anaweza kupunguza kidogo bei ya gari lake, ile magurudumu yabadilishwe mazuri.
G- Ni lazima kubadili magurudumu mawili tu. Kila mwaka makanika alikuwa anaangalia gari langu zima.
J- Nikibadili magurudumu mawili tu nitakuwa na ajali. Makanika wako amebadili magurudumu kweli?
G- Miaka miwili iliyopita nilibadili magurudumu yote, lakini ni lazima kubadili magurudumu mawili tu, tayari nilishasema hayo.
J- Unataka kuniibia sasa ninaweza kulipa pesos elfu ishirini na nane, na tafadhali uitike swali langu, makanika wako alibadili magurudumu?
G-Makanika wa gari langu ni bora kuliko wote wengine, lakini yeye hakubadili magurudumu. Warsha ya mitambo ambapo nilipeleka gari langu, utaalamu wake haswa ni magurudumu.
A- Nafikiri kwamba magurudumu si tatizo lenye umuhimu sana. Nasema tena, Gaby anaweza kupunguza bei ya gari na Javier anaweza kubadili magurudumu mawili baadaye. Mtambo ni muhimu zaidi, hali ya mtambo wa gari lako ni nini?
G- Mtambo ni mpya, mnataka kuiona? Na ndiyo, ninaweza kupunguza bei kwa matatizo ya magurudumu, lakini siwezi kupunguzia bei hadi ile aliyosema Javier.
A- Javier labda unaweza kujaribu gari lake ili uone kwamba gari linatembea vizuri.
J- Nina wasiwasi kuhusu kuendesha gari hili kwa sababu makanika na watu wanaofanya kazi warshani mwa Gaby si watu waaminifu.
A- Acha kuzungumza maneno yasiyo na maana na kuendesha au kutafuta gari lingine.
J- Ninaweza kuendesha lakini nikifa Gaby atakuwa na tatizo kubwa.
G- Ninafikiri haendeshi gari la miongozo kwa hivyo Javier ana wasiwasi.
J- Ninajua kuendesha gari la aina hilo lakini hilo si gari ninalotafuta kwa sababu goti langu la kushoto linauma sana.
A- Ungalisema hivyo tangu mwanzo. Ulifanya tupoteze muda wetu bure. Samahani Gaby, Javier hajui anachotaka.
G- Hakuna matata, lakini sitaki kumwona rafiki yako tena.
J- Kwa herini.

*Esta web está en continuo desarrollo, siendo actualizado su contenido periódicamente, por lo que progresivamente va ampliando el material publicado. 

colmex-swahililogo ceaa 50 

© 2015 El Colegio de México, A.C.