Skip to main content

Chakula cha Mehiko

Chakula cha Mehiko

6. Mazoezi ya Kusikiliza (Comprensión Oral) 1

Javier Sacristán de Alva

Nchini Mehiko kuna chakula kilicho na historia nyingi. Tangu zamani, yaani kabla ya wazungu kufika nchini kwetu, kiambato kilichokuwa na muhimu sana kimekuwa mahindi. Watu wa wakati huo walichemsha mahindi ili wayapike. Pia kuna vyambato kama pilipili, boga, nyanya na kadhalika vilivyotumika. Kuna wanyama waliofugwa, kwa mfano, kuchakuro, nyoka na mbwa. Pia watu walifuga wadudu.

Mmea wa cacao ulitumika kama pesa wakati huo. Kiongozi kama Moctezuma, kwa mfano, alitumia huo kama pesa zake. Wazungu waligundua mmea wa cacao mnamo karne kumi na sita wakati Colon alipofika Amerika. Pia Wamehiko wa bonde la Mehiko walitumia cacao ili kutengeneza kinywaji cha kuwachangamsha kwa sababu hiyo cacao ina umuhimu mno.

Sasa chakula kina umuhimu sana katika utamaduni wa Wamehiko kwa ujumla. Tuna methali zingine zinazoweza kuonyesha hivyo kwa mfano: “wakati kichwa kinapoumwa ni wakati wa kula” au “batamzinga aondokaye bomani ataishia kwenye mole”. Methali hizo zinahusiana na tabia za watu huko zikitumia chakula ili kuonyesha masomo ya kimaisha.

Mole ni chakula kimojawapo cha desturi huko Mehiko, ijapokuwa si rahisi kuipika kwa sababu ni lazima mpishi atumie vyambato vingi. Neno la mole linatoka kinahuatl lakini wazungu walikuwa wa kwanza wa kutengeneza chakula hicho. Watu wengi wanasema kwamba mtu ambaye alikuwa wa kwanza kuitengeneza mole aliitwa Pascual na alikuwa mtawa wa kiume. Pascual alitengeneza mole kwa sababu alitegemea kutembelewa na mfalme msaidizi aliyeitwa Juan de Palafox. Pascual alikuwa mpishi wa utawa wake wa kiume na alikuwa na wasiwasi kuhusu ziara ya mfalme msaidizi kwa hivyo alijaribu kuokoa vyambato lakini alijikwaa na hivyo vilianguka ndani ya chungu iliyokuwa na batamzinga kwenye maji ya moto. Vyambato hivyo vilikuwa kakao, pilipili, na viungo vingine.

Chakula cha Mehiko hutumia sana pilipili na mahindi. Watu wengi pia hutumia tortilla kama kijiko ili kula chakula chao. Tortilla ni kama chapati ya mahindi. Watu wanaweka chakula ndani na tortilla inafanyiwa gombo; hiki kinaitwa taco.

Pia Wamehiko hula wadudu, kuna spishi mia tano arobaini na tisa za wadudu mtu anayeweza kula. Watu wengine wanafikiri kwamba hivyo vinakirihi na kuna wengine ambao hupenda chakula hicho. Wadudu wanao protini kwa hivyo kwa muda mrefu Wamehiko wametengeneza chakula kilicho na wadudu.

Sasa kuna watu wengi wanaokula barabarani kwa sababu ya vyakula kama tacos, tamales, na kadhalika ambavyo ni rahisi sana. Wafanyakazi wana saa moja tu ili wale kwa hivyo wanatafuta chakula chinachopikwa kwa haraka na pia chenye bei rahisi.

Tamal ni neno la kinahautl linalomaanisha kuzungushia, hiyo ina mahindi na nyama au matunda. Hatujui ni katika nchi ipi watu walianza kutayarisha tamal kwa sababu nchi nyingi za Amerika zina chakula hicho. Lakini mahindi yanatoka Mehiko. Kwa sababu hiyo kunawezekana kwamba Wamehiko walikuwa wa kuanza. Mehiko ina aina nyingi za tamal, kuna tamal za rangi nyingi. Bernardino de Sahagun aliandika Historia ya Uspeni Mpya, kitabuni huko, alitaja tamal kuwa chakula chenye umuhimu.

Watu wengi hula tacos za “pastor” yaani za “mchungakondoo”. Chakula hicho kina nyama ya nguruwe na nanasi. Vijana wanaenda kula hicho baada ya sherehe kumalizika na wakiwa na njaa. Unaweza kula hicho pembeni ya barabara au katika masoko mengi, lakini ni lazima uangalie vizuri pahala utakapokula kwa sababu mara kwa mara watu wanaotayarisha chakula hawaoshi vyema vyombo vyao.

  1. Ili utengeneze mole, lazima utumie vyambato gani?
  2. Wazungu ni lini waligundua kakao?
  3. Methali zinazotumika hapa ni zipi?
  4. Maoni mawili yaliopo kuhusu kula wadudu ni yapi?
  5. Pascual alikuwa nani?
  6. Mwandishi anataja vyambato vipi vlivyokuwepo kabla ya wazungu kufika Mehiko?
  7. Kwa nini cacao ilikuwa na umuhimu?
  8. Kwa nini mole ilitengenezwa mara ya kwanza?
  9. Wamehiko walitumia cacao ili watengeneze nini?
  10. Watu wanatumiaje tortilla ili kutengeneza chakula?