Skip to main content

Mapinduzi ya Mau Mau

Mapinduzi ya Mau Mau

16. Monologia (lección y comprensión) 3

Javier Sacristán de Alva

Historia ina umuhimu katika maisha ya wote kwa sababu wanaweza kusoma kuhusu mambo yanayobadilika duniani, kwa mfano vita, mapinduzi, na pia vitendo walivyofanya wanaserikali. Historia ya Kenya ina manufaa kwa Mkenya anayeisoma kwa makini ili aelewe kwamba watu walioungana kupigana na wazungu bado wana matatizo mengi katika siasa

Mapinduzi ya Mau Mau yalianza mnamo mwaka elfu moja mia tisa hamsini na mbili na yalimalizika mnamo mwaka elfu moja mia tisa hamsini na sita. Ninatumia kipindi hicho kwa sababu elfu moja mia tisa hamsini na sita ni mwaka Waingereza walipomwua Dedan Kimathi lakini kuna wanahistoria wengi wanaosema kwamba yalimalizika mwaka elfu moja mia tisa sitini kwa sababu wafungwa waliokuwa kambini walirudia nyumbani kwao mwaka huo. Pia, kuna wananchi wa Kenya wanaosema kwamba hata leo kuna Mau Mau msituni wanangojea wakati watakapoweza kurudi ili kupigana tena.

Mau Mau si jina la Kiafrika ni jina la Kizungu lililotungwa ili watu wote dunia nzima wafikiri kwamba Wagikuyu walikuwa kama wanyama. Wakenya waliwaita washirika wa mapinduzi hayo: Jeshi la Shamba na Uhuru. Watu walioanza kupigania uhuru mwanzoni walikuwa wanataka Waingereza wawarudushie Wagikuyu mashamba yao yaliyokuwa yameibwa.

Dedan Kimathi ni mtu ambaye alikuwa na umuhimu mno katika mapinduzi hayo kwa sababu aliandika mengi kuhusu mambo wapiganaji waliofanya wakati wa mapinduzi, pia aliandika makanuni; kwa mfano aliwashawishi wana Mau Mau wasinywe pombe. Waingereza walitaka kumwua kwa sababu alikuwa ana mafunzo ya jeshi kutokana na kipindi alipopigana pamoja na jeshi la Uingereza wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na pia alikuwa na itikadi kali.

Kuna watu walioanza kupigana kama wanajeshi wa Mau Mau lakini baada ya kufungwa na Waingereza walianza kuwasaidia Waingereza hawa. Mfano moja ni General China. Waingereza walimkamata mwaka elfu moja mia tisa hamsini na nne na walimhukumu na kifo cha kunyongwa, lakini hao walisema kwamba wapiganaji watakaoacha kupigana watapewa msamaha. Kwa sababu hiyo China alisema kwamba wakati Waingereza walipomkamata alikuwa anaenda kuwapa silaha zake. Waingereza walimsamehe maisha yake lakini ilikuwa lazima awaandikie viongozi wa wapiganaji wengine kama Dedan Kimathi ili waache kupigana nao. Dedan Kimathi alijibu barua la General China na kumwambia kwamba ataanza kuzungumza kuhusu kuacha kupigana ambapo Waingereza watatoka Kenya na kuwarudishia Wagikuyu mashamba yao.

Watu waliowasaidia Waingereza walikuwa na ahadi ya kwamba vita hivi vitakapomalizika watakuwa na mashamba mengi. Wakenya walipigana na Wakenya na Waingereza walibaki kuwaangalia.

Jomo Kenyatta, rais wa kwanza wa Kenya alikuwa gerezani wakati wa mapinduzi kwa sababu Waingereza walifikiri kwamba alikuwa anaongoza Mau Mau, lakini ukweli ni kwamba hakutaka kuwakabili Waingereza kwa ukali. Vijana waliopigana Vita vya Pili vya Dunia walifikiri maisha yatapata afueni watakaporudi Kenya baada ya vita hivyo lakini haukutokea na kwa hivyo walianza mapinduzi dhidi ya wakoloni.

Baada ya mapinduzi kumalizika, Kenyatta aliachiliwa uhuru na alianza kusema kwamba Mau Mau ilikuwa kama ugonjwa wa Kenya na kutaka Wakenya waisahau historia yao na kutazama wakati ujao. Watu ambao waliendelea kuzungumza au kuandika kuhusu Mau Mau kama Ngugi wa Thiong’o au Tom Mboya waliuawa au kufungwa gerezani.

Sasa watu waliopigana mapinduzini wanadai haki zao katika Mahakama ya Mataifa dhidi ya Uingereza. Wao walitaka serikali ya Uingereza iwalipe kwa sababu ya muda walipokuwa gerezani wakiwa wanateswa. Watu waliowatesa wapiganaji hawa si Waingereza ni Wakenya lakini Waingereza waliwashurutisha wafanye hivyo. Hayo ni yanayosababisha shida nyingi za kisasa, kwa sababu mtu aliyepigana na Waingereza akitembea huweza kumwona mtu aliyemtesa na kufikiri kwamba ni lazima awe gerezani.