Skip to main content

Asasi na Les Ballets Africains ya Guinea

Asasi na Les Ballets Africains ya Guinea

10. Monologia (lección y comprensión) 2

Adriana Gabriela Bañales De León

Les Ballets Africains ya Guinea ni kampuni lililokuwa la kwanza ambalo lilitoka barani Afrika kucheza madansi ya Guinea. Baada ya Guinea kupata uhuru wake kampuni hili likawa alama ya taifa duniani kote. Kwa vyo vyote historia ya Les Ballets ilianza miaka kadhaa kabla ya tukio hili, mnamo elfu moja mia tisa hamsini na nane.

Fodeba Keita, mzaliwa wa Guinea, ni mtu aliyejifunza sheria Paris. Pamoja na Kante Facelli, aliyekuwa griot, waliunda kampuni la kucheza dansi mnamo elfu moja mia tisa arobaini na saba, lakini wakati huo liliitwa L’ensemble de Fodeba-Fancelli Moungaré. Hapo awali lilikuwa linajihusisha na watu wa Afrika bara nzima, wa Marekani na pia watu waliotoka Visawe vya Karibi; wao wote, ambao walikuwa wanaume watupu, walicheza dansi na kupiga muziki kutoka Guinea, Mali, Côte d’Ivoire, Kongo, Senegal na labda Visawe vya Karibi. Kwa muda mfupi, takriban miaka mitano, maonyesho yao yalitolewa kwa ajili ya waafrika walioishi Ulaya, lakini Wazungu walikuwa na nia pia ya kuona maonyesho hayo.

Mnamo mwaka elfu moja mia tisa hamsini na mbili kampuni lilibadili jina lake kuwa Les Ballets Africains de Keïta Fodeba. Pia kulikuwa na mabadiliko mengine; kwa mfano, kwa mara ya kwanza kampuni lilikuwa na mchezaji wa ngoma wa kike aitwaye Leila Mondor (Cohen 2012:25). Maonyesho ya kampuni kwa hivi sasa yalikuwa na lengo la kuwavutia Wazungu. Mwaka uliofuata Fodeba Keita alisafiri Afrika ya Magharibi ili kutafuta wanamuziki na wachezaji wapya, kutokana na hilo kampuni hili lilianza kujihusisha na watu waliotoka Afrika ya Magharibi pekee yake. Kutoka mwaka huu Les Ballets lilikuwa na maonyesho kote Ulaya. Muziki na madansi yaliyopigwa katika maonyesho yao aghalabu yalikuja kutoka kabila la Wamalinke.

Kampuni liliwaajiri wanamuziki na wachezaji zaidi kutoka Afrika ya Magharibi mwaka elfu moja mia tisa hamsini na sita. Lilisafiri Senegal, Mali, Burkina Faso, Nijer, Benin, Côte d’Ivoire na Guinea ili lifanye maonyesho yao. Kampuni pia lilisafiri baadhi ya nchi za Amerika ya Kusini, Uyahudi na Uturuki mwaka uliofuata. Wakati wa ziara hizi, kampuni lilikuwa na matatizo kadhaa kutokana na jinsi wachezaji wanawake walivyovaa mavazi yalionyesha mwili karibia mzima. Mjini New York lilikuwa na maonyesho arobaini Broadway na mwezi wa pili lilifanya onyesho katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwaka elfu moja mia tisa hamsini na tisa. Kampuni lilipomaliza ziara hii lilibadili makao makuu yake kutoka Paris hadi Conakry kwa mwito wa Sékou Touré ambaye alikuwa rais wa Guinea wakati ule.

Mwaka elfu moja mia tisa sitini ulikuwa mwaka muhimu sana kwa sababu kampuni likawa mwakilishi wa Jamhuri ya Guinea nje ya nchi yake. Hilo lilimaanisha kwamba kampuni lilikuwa na ushirikiano mdogo katika maisha ya muziki ndani ya nchi ya Guinea. Kwa hivyo lilibadili jina lake tena na kuwa “Les Ballets Africains de la République de Guinée”. Kutokana na hilo kulikuwa lazima wanachama wote wa kampuni wawe wananchi wa Guinea tu. Mwaka huu Fodeba Keita alimpa Kante Fanccelli uongozi wa kampuni kwa sababu Keita alianza kuwa Waziri wa Ulinzi na Usalama nchini Guinea.

Wakati wa serikali ya Sékou Touré hata siku za leo Les Ballets Africains de Guinea limepata kufahamika na kuongezea umashuhuri duniani kote. Hayo yaliwaruhusu wanamuziki na wachezaji waliyotoka kampuni hilo kufundisha mahadhi yao katika nchi nyingine nyingi, hasa nchi za Ulaya na Marekani. Les Ballets limekuwa mwakilishi wa serikali ya Guinea na wananchi wa nchi hii pia.

Marejeo

  • COHEN, Joshua. “Stages in Transition: Les Ballets Africains and Independence, 1959 to 1960”. Katika Journal of Black Studies, 43 (1). 2012. Pp. 11-48.

  • SAÏDOU, Marceline. “Cultural Nationalism in Guinea and Les Ballets Africains, 1947-1967“. Mwezi wa kumi na mbili, 2000. Pp. 22. Makala ambayo haijachapishwa.